Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema uongozi wa timu hiyo unazo taarifa kuwa kuna timu zinajaribu kutumia njia za mkato kuwasajili wachezaji ambao bado wana mkataba na klabu ya Yanga.
Ten amezitaka timu hizo zinazotaka wachezaji wa Yanga zifike Makao Makuu ya klabu hiyo kuonana na uongozi badala ya kutumia utaratibu ulio kinyume na sheria.
Kumekuwa na taarifa kuwa Simba inajaribu kila namna kumsajili kiungo Papi Kabamba Tshishimbi ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Yanga.
Ten amesema ni vyema viongozi wa timu hiyo wakawasiliana na uongozi wa Yanga kama kweli wanamtaka mchezaji huyo na wasijaribu kutumia njia za mkato.
Kwa mujibu wa sheria za usajili za FIFA timu moja hairuhusiwi kufanya mazungumzo na mchezaji wa timu nyingine ambaye bado ana mkataba unaozidi miezi sita.
Kwa wachezaji ambao mikataba yao ni chini ya miezi sita ndio wanaoruhusiwa kufanya mazungumzo na hata kusaini mikataba ya awali.

ADVERTISE HERE