Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union hapo jana katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma, kikosi cha Yanga kimeondoka Dodoma kurejea Dar.
Kwa sasa ligi inakwenda kusimama kwa takribani wiki sita kupisha michuano ya Afcon 2025 inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu huko Morocco.
Nyota walioitwa timu za Taifa wanakwenda kujiunga na mataifa yao kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo.
Uongozi wa Yanga unatarajiwa kutoa mapumziko ya siku chache kwa wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za Taifa kabla ya kurejea kuendelea na maandalizi.
Mchezo utakaofuata baada ya michuano ya Afcon kumalizika ni dhidi ya Al Ahly, ugenini huko Misri Januari 23 2026 ligi ya mabingwa





ADVERTISE HERE