Ule msemo 'usimkatie mtu tamaa' una maana kubwa sana kwa mshambuliaji wa Yanga Prince Dube ambaye jana aliwahakikishia Wananchi ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Dube alifunga bao pekee kwenye dakika ya 88 akimalizia krosi ya Duke Abuya kutokea upande wa kulia.
Dube alianza msimu vibaya akikumbana na ukosaji mkali kutoka kwa wachambuzi na kupelekea presha kubwa ambayo kama sio mashabiki wa Yanga kuwa nae katika nyakati zote pengine angeshapotea.
Pamoja na kuwa bado hajafikia matarajio ya Wananchi kwa asilimia 100 lakini amekuwa mchezaji muhimu katika nyakati muhimu kwa Yanga.
Baada ya ukame wa muda mrefu, akafunga bao pekee katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya AS FAR na kuipa Yanga ushindi wa bao 1-0.
Katika mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Fountain Gate, Dube alifunga bao la kwanza kupitia mkwaju wa penati kabla ya Pacome Zouzoua kuongeza la pili.
Jana baada ya kupoteza nafasi kadhaa, akasahihisha makosa yake dakika za jioooni na kuifungia Yanga bao lililowahakikishia Wananchi alama tatu zilizowasogeza hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 16.
Huyu ndiye Mwana Mfalme ambaye msimu huu amepachika mabao manne kwenye mashindano yote