Yanga kuanza na straika huyu dirisha dogo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Dec 2025
Yanga kuanza na straika huyu dirisha dogo

Tetesi tayari zimeanza kushika kasi kuelekea dirisha dogo la usajili ambalo linatarajiwa kufunguliwa wiki ijayo Disemba 15 na kuwa wazi hadi Januari 16 2026.

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amethibitisha kuna maboresho yatafanyika dirisha dogo ili kuimarisha maeneo yaliyoonekana kuwa na changamoto kwa kuzingatia mapendekezo ya benchi la ufundi.

Eneo la kwanza ambalo limezungumzwa sana na mashabiki wa Yanga ni safu ya ushambuliaji, ikielezwa ni eneo pia ambalo mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves amependekeza kuongezweza nguvu.

Jina la mshambuliaji Laurindo Dilson Maria Aurelio aka DEPU limetajwa kuwa pendekezo la kwanza la Goncalves.

Depu raia wa Angola, anaitumikia klabu ya Radomiak inayoshiriki ligi daraja la kwanza huko Poland. Nyota huyo amewahi kupita kwenye vilabu vya Petro de Luanda ya Angola, Gil Vicente ya Ureno na Vojvodina ya Serbia.

Pia Depu ameitumikia timu ya Taifa ya Angola ambapo ameifungia magoli 15 kwenye mechi 18 wakati huo ikinolewa na Goncalves.

Hata hivyo endapo Yanga itamsajili Depu huenda ikalazimika kukata jina la mchezaji mmoja wa kigeni ili kuitumia nafasi yake.

Na wakati huohuo pia Yanga itahitaji nafasi nyingine ili kumsajili beki Yao Kouassi ambaye yuko tayari kurejea kikosini baada ya kupona majeraha.

Maeneo mengine yanayotajwa kuhitaji maboresho ni kiungo mkabaji na kiungo wa ushambuliaji (namba 10).

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’