Kiungo wa Yanga Duke Abuya yuko kwenye orodha ya wachezaji waliotoa pasi nyingi za mabao katika ligi kuu ya NBC msimu huu.
Abuya ambaye kwa sasa anatumika kama kiungo mkabaji, ametoa pasi tatu za mabao akiwa sawa na Raymond Chamungu (Namungo) na Elie Mpanzu (Simba).
Aina yake ya uchezaji inamfanya kuwa kila mahali uwanjani, ni wazi msimu huu atafanya mambo makubwa zaidi.

ADVERTISE HERE