Lema ang'oa mwingine Msimbazi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Dec 2025
Lema ang'oa mwingine Msimbazi

Kocha Mkuu wa Yanga Princess Edna Lema ameanza mapema kufanya maboresho ya kikosi chake kuelekea kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili siku chache zijazo.

Msimu huu Yanga Princess imekataa unyonge kwani Lema analitaka taji la ligi kuu ya Wanawake kwa mara ya kwanza.

Tayari Wananchi wamemalizana na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba Queens Asha Djaffar raia wa Burundi.

Djafar aling'ara na kikosi cha Simba Queens kwa misimu kadhaa, anasubiri kuanza kuwatumikia Wananchi utambulisho wake umefanyika leo.

Yanga Princess itashuka dimbani kesho Ijumaa kuikabili Tausi katika mwendelezo wa ligi kuu ya Wanawake.

Djaffar huenda akaanza kuonekana kikosini baada ya usajili wake kukamilika pale dirisha dogo litakapofunguliwa Disemba 16.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’