Yanga kuketi na waliomaliza mikataba leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 May 2018
Yanga kuketi na waliomaliza mikataba leo
Uongozi wa Yanga leo utafanya kikao na wachezaji ambao mikataba yao ya kuitumikia timu hiyo imemalizika na wale ambao mikataba yao inamalizika hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa ametoa taarifa hiyo mapema leo muda mfupi baada ya kusambaa uvumi kuwa beki Kelvin Yondani ambaye ni miongoni mwa waliomaliza mikataba, hajulikani alipo.

Yanga ina wachezaji 10 waliomaliza/wanaomaliza mikataba yao ambao ni Benno Kakolanya, Hassani Kessy, Juma Abdul, Kelvin Yondani, Andrew Vicent, Nadir Haroub, Said Juma Makapu, Obrey Chirwa, Geofrey Mwashiuya na Emanuel Martin.

Mkwasa amesema wanakusudia kumalizana na wachezaji hao kabla ya kwenda nchini Kenya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza Juni 03 mpaka Juni 10.

Yanga itafungua mashindano hayo kwa kucheza na KK HomeBoyz Juni 03 mchezo utakaopigwa saa saba mchana.

Mabingwa hao wa kihistoria wa soka Tanzania, wanatarajiwa kuondoka kesho May 31 kuelekea nchini Kenya.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’