Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), limemteua Rais wa Klabu ya Yanga na Mwenyekiti wa Umoja wa vilabu Afrika (ACA), Injinia Hersi Said kuwa miongoni mwa wataalam watakaofundisha kwenye kongamano kubwa la Mpira litakalofanyika Doha, Qatar, siku ya Jumapili, Desemba 14,2025.
Hersi amepangiwa na FIFA kufundisha kwenye mada ya mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu.
Miongoni mwa Wataalam wengine wa mpira Duniani watakaozungumza kwenye Kongamano hili ni Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger, Roberto Di Mateo, Dennis Wise, Alexander Pato na Eric Abidal.
Hersi ni mtaalamu pekee wa mpira kutoka Afrika aliyepata nafasi ya kufundisha Kwenye Kongamano hilo.
ADVERTISE HERE