Kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kurejea mazoezini baada ya mapumziko ya wiki moja.
Licha ya ligi kusimama kwa takribani wiki sita kupisha michuano ya Afcon 2025 inayotarajiwa kuanza wiki ijayo huko Morocco, mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves ameandaa program maalum za mazoezi ili kuhakikisha wachezaji wake hawakai muda mrefu bila kufanya mazoezi.
Baada ya kurejea mazoezini, Yanga itajifua kwa takribani wiki moja na kisha kwenda kwenye mapumziko ya sikukuu ya Christmass.
Aidha kutokana michuano ya kombe la Mapinduzi kutarajiwa kuanza Disemba 29, huenda program hiyo ikabadilika hasa ikizingatiwa Yanga ni miongoni mwa timu zitakazoshiriki michuano hiyo.
Awali baada ya mapumziko ya xMas, Yanga ilitarajiwa kurejea tena mazoezini Disemba 29.
ADVERTISE HERE