Nililenga kutoa elimu ya mabadiliko - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Dec 2025
Nililenga kutoa elimu ya mabadiliko - Hersi

Rais wa Yanga na Mwenyekiti wa Chama cha Klabu za Soka Afrika (ACA), Injinia Hersi Said amesisitiza klabu za Afrika zinapaswa kumaliza changamoto za kiutawala, miundombinu na udhamini ili kupiga hatua kubwa za maendeleo.

Hersi ametoa kauli hiyo baada ya mjadala mkali kuibuka kufuatia kile alichozungumza hivi karibuni kwenye kongamano la soka lililoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) huko Qatar.

Hersi amesema hakuwa na lengo la kuidharirisha timu yoyote katika kongamano hilo bali mchango wake ulilenga kuonyesha namna klabu nyingi Afrika zinavyokabiliana na udhaifu mbalimbali, matatizo ya kiutawala, miundombinu na udhamini unaojitosheleza.

“Nimezungumzia maendeleo ya klabu na mabadiliko yake ya kiungozi, eneo la kwanza nilizungumzia changamoto za eneo hilo, huwezi kukimbia uongozi bora unaopaswa kuziendesha klabu zetu, nikatoa mifano ya klabu zetu nikianza na Yanga tulipotoka tena tukaonyesha video za vikao vya wanachama wetu kabla ya mabadiliko ya kiuongozi, baada ya hapo tukaonyesha mambo yanayoendelea kwa wenzetu wa Simba."

“Nataka kukuambia huko nyumbani mnajadili mambo mepesi lakini wenzetu huku wameelimika sana na namna klabu zetu za Afrika zinahitaji kubadilika kiutawala, hatuwezi kufikia hatua kubwa kama tutaendelea kukabiliana na changamoto za kiutawala.”

Aidha, Hersi alifafanua kuwa eneo la miundombinu nalo ni sehemu ambayo klabu zinatakiwa kubadilikapia mfano wake ulionyesha namna Yanga ilivyokuwa na jengo dhaifu mpaka kulibadilisha na kuwa la kisasa.

“Kuna eneo la miundombinu, tukubalieni tuna deni kubwa la kutakiwa kubadilika hapa, pale nikaonyesha picha ya jengo letu la klabu kabla ya kufanyiwa marekebisho makubwa, kupitia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji (transformation), nikaonyesha picha za klabu yetu na jengo letu kabla, husikii watu wa Yanga wakilalamika.

“Utazungumzia kuhusu maendeleo ya kisoka, na soka la vijana, mifumo sahihi ya kuendeleza wachezaji na hasa wadogo wa kiume na wale wa kike hizi ndizo changamotio za klabu zetu hapa Afrika.

“Baada ya kuona hayo, eneo la pili tukaangalia ni njia gani sahihi, nikaeleza njia sahihi ni kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu zetu, tulete uongozi ambao una mfumo mzuri, tulete wataalam waingie kwenye mpira, tutafute wadhamini kwani klabu zetu bado zinahitaji sana wadhamini ili ziweze kumudu kujiendesha, haya yanaweza yote yataweza kuchangia maendeleo ya mpira wa Afrika.

“Eneo la tatu tukaonyesha faida ya mabadiliko ya kiuongozi ambayo klabu yetu imeanza kuyapitia. Mfano sisi Yanga kupitia mabadiliko haya tulikuwa tunaingiza kiasi cha Sh10 milioni kwa mwaka lakini sasa unazungumzia klabu kuingiza kiasi cha Sh1.3 bilioni, tulikuwa na wanachama hai wasiozidi 1,000 lakini sasa tumefikisha wanachama hai zaidi ya 90,000, tunaingiza fedha nyingi na bado tunaweza kufanya zaidi, nadhani nyie wanahabari mliona kwenye mkutano wetu mkuu uliopita.”

Hersi aliongeza kuwa hana shida na uongozi wa Simba wala klabu hiyo, lakini mchango wake ulilenga kuzisaidia klabu zote hatua ambayo ilipokewa na mlengo chanya na mkutano huo.

“Nawaheshimu sana Simba, kuanzia mwenyekiti wake Murtaza Mangungu, mwenyekiti wa bodi Magori (Crescentius) nadhani hata wao mkiongea nao watakiri hizo ni changamoto kubwa za klabu zetu, sisi tumekabiliana nazo na tunaendelea na hata wao wanakabiliana nazo,” alisema.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’