Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili salama Morocco kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zinazotarajiwa kuanza Jumapili, Desemba 21.
Stars imewasili ikitokea Cairo, Misri ambako iliweka kambi ya maandalizi kwa takribani wiki mbili na kucheza mechi za kirafiki.
Nyota wanne wa Yanga watakuwa sehemu ya kikosi cha kocha Miguel Gamondi ambaye katika michuano ya mwaka huu ameahidi kuiongoza Stars kufika hatua ya mtoano.
Mohamed Hussein, Ibrahim Bacca, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto wamejumuishwa katika kikosi hicho.
Taifa Stars imepangwa Kundi C na itaanza kampeni yake Jumanne, Desemba 23 dhidi ya Nigeria ‘Super Eagles’, ikisaka matokeo chanya ya kihistoria katika michuano hiyo.
Ratiba ya mechi za Taifa Stars AFCON 2025 (Kundi C)
- Desemba 23: Tanzania vs Nigeria
- Desemba 27: Tanzania vs Uganda
- Desemba 30: Tanzania vs Tunisia