Michuano ya Afcon 2025 ilianza kutimua vumbi jana kwa wenyeji Morocco kuanza vyema michuano hiyo kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Comoros.
Michuano hiyo inaendelea leo ambapo mechi nne zitarajiwa kupigwa huku Tanzania ikitarajiwa kushuka dimbani kesho Jumanne.
Nyota wawili wa Yanga leo watakuwa dimbani kuzitumikia timu zao za Taifa katika michuano hiyo.
Mlindo lango Djiguo Diarra anatarajiwa kuiongoza Mali katika mchezo dhidi ya Zambia utakaopigwa saa 11 jioni.Diarra huenda akakumbana uso kwa uso na mshambuliaji wa zamani wa Yanga Kennedy Musonda ambaye amejumuishwa katika kikosi cha Zambia.
Majira ya saa 5 usiku, Prince Dube na timu yake ya Taifa ya Zimbabwe atakuwa na kibarua kigumu mbele ya Misri katika mchezo wa mwisho siku ya leo.

Timu ya Taifa ya Tanzania itashuka dimbani kesho kumenyana na Nigeria katika mchezo utakaopigwa saa 2:30 usiku.