Yanga haijawahi kutishiwa 'nyau'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
31 May 2018
Yanga haijawahi kutishiwa 'nyau'
Msimu huu wa 2017/18 ni moja ya misimu ambayo Yanga imekuwa katika kiwango cha chini zaidi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Matatizo yaliyompata Yusuph Manji, aliyekuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Yanga ambayo yalipelekea ajiuzulu, ndiyo chanzo cha hali 'mbaya' ya kiuchumi iliyoharibu 'mambo' Jangwani

Wakati huu ambao msimu umemalizika bado kuna sintofahamu juu ya zoezi la usajili ikielezwa kuwa huenda wachezaji muhimu ambao mikataba yao imemalizika wataondoka.

Juma Abdul, Kelvin Yondani na Obrey Chirwa wanatajwa kuwa mbioni kuachana na Yanga.

Juzi nilimsikia Afisa Habari wa Simba Haji Manara akitamba kuwa mwaka huu wamedhamiria kuibomoa Yanga.

Ngoja niwakumbushe jambo. Mwaka 1994 Yanga ilikumbwa na mgogoro uliokuwa maarufu kati ya 'Yanga Kampuni' na Yanga Asili' uliovuruga mustakabali wa timu.

Mgogoro huu ulitokea baada ya kuwepo kwa makundi mawili, moja likitaka mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Yanga kuwa Kampuni na jingine likipinga mabadiliko hayo 'Yanga Asili'.

Kutokana na mvutano uliojitokeza baadhi ya wachezaji waandamizi walijikuta wakiingizwa kwenye mgogoro huo na wakatumiwa kuihujumu timu.

Baada ya kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Simba mwaka 1994, ndipo Kocha Mkuu wa Yanga wakati huo, Tambwe Leya alipoamua kuivunja timu na kusajili upya kwa kuendesha zoezi la usaili wa wachezaji na wengine akiwapandisha kutoka Yanga B.

Kikosi hicho kipya cha Tambwe Leya kilichokuwa kimesheheni vijana wadogo kilipachikwa jina la Black Stars.

Miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye kikosi hicho ni pamoja na Anwar Awadh, Mzee Abdallah, Silvatus Ibrahim “Polisi”, Maalim Saleh “Romario”, Nonda Shaaban “Papii” na wengine.

Pia baadhi ya wachezaji wakongwe waliobaki katika kikosi hicho ni pamoja na Sekilojo Chambua, Salvatory Edward na Bakari Malima 'Jembe Ulaya'.

Wachezaji 'wakubwa' ambao walionyeshwa mlango wa kutokea ni pamoja na kipa Rifat Said aliyerudi Zanzibar, Edibily Lunyamila aliyekwenda pia Malindi ya Zanzibar, Saidi Mwamba 'Kizota' na Steven Nemes waliohamia Simba.

Ni vijana hawa ambao baadae walikuja kuijenga Yanga imara iliyotinga robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika mwaka 1998 wakati huo ikishirikisha timu nane.

Pia ni hawahawa waliofanikiwa kubeba ubingwa wa Afrika Mashariki na kati nchini Uganda mwaka 1999 na kutumiwa Ndege na Serikali kisha kupokelewa uwanja wa Ndege na Waziri Mkuu wa wakati huo Fredrick Sumaye.

Hii ndiyo Yanga iliyomtoa mchezaji aliyekuja kuwa maarufu sana duniani, Nonda Shaabani 'Papii'aliyetamba nchini Ufaransa na Uingereza.

Na hii haikuwa mara ya kwanza kwa Yanga kufanya hivyo. Zoezi kama hilo lilifanyika mwaka 1972.

Hivyo historia inaonyesha hakuna namna Yanga inaweza kubomolewa, hata wakiondoka wachezaji wote leo, Yanga itabaki imara.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →