Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves ni kocha pekee katika ligi kuu ya NBC mpaka sasa hajapoteza mchezo.
Pedro ambaye ameiongoza Yanga katika michezo minne kwenye ligi kuu ya NBC, ameifanya vyema kazi iliyoachwa na mtangulizi wake Romain Folz ambaye aliongoza michezo miwili ya kwanza akishinda mmoja na kutoa sare 1.
Goncalves katika michezo minne, ameshinda michezo yote akiwa amevuna alama 12 na kufunga magoli 9 na kuruhusu goli moja pekee.
Alifungua ukurasa wake katika ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar na kupata ushindi wa 2-0, akawafunga KMC 4-1, akawakaribisha Fountain Gate na kushinda 2-0 kabla ya kuelekea Dodoma na kupata ushindi wa dakika za jioni dhidi ya Coastal Union kwa 1-0.
Makocha wengine walioshinda michezo sawa na Goncalves ni Ahmad Ally wa JKT Tanzania na Francis Baraza wa Pamba Jiji ambao wameshinda michezo minne huku wao wakiwa tayari wamepoteza mchezo mmoja mmoja na kupata Sare katika michezo yao mingine iliyosalia.