Dube dimbani kuwakabili Angola, Diarra Morocco

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Dec 2025
Dube dimbani kuwakabili Angola, Diarra Morocco

Baada ya mapumziko ya sikukuu ya Christmas, michuano ya Afcon 2025 inaendelea leo ambapo mchezo wa mapema saa 9:30 alasiri Zimbabwe itachuana na Angola.

Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube ambaye alifunga bao pekee la Zimbabwe katika mchezo uliopita waliopoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Afrika Kusini, atakuwa na jukumu la kuibeba Zimbabwe katika mchezo mwingine muhimu.

Nyota mwingine wa Yanga Djigui Diarra yeye atakuwa na mtihani mgumu zaidi pale timu yake ya Mali itakapokabiliana na wenyeji Morocco katika mchezo utakaopigwa saa 5 usiku.

Mali walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Zambia katika mchezo uliopita.

Kesho Jumamosi timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itashuka dimbani kumenyana na Uganda, mastaa wengine wa Yanga Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Mohammed Hussein wakitarajiwa kushuka dimbani.

Baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Nigeria, mchezo dhidi ya Uganda ni lazima kwa Tanzania kushinda ili kuweka hai matumaini ya kutinga hatua ya mtoano.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
57m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’