Afcon 2025 : Gamondi apania ushindi dhidi ya Uganda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Dec 2025
Afcon 2025 : Gamondi apania ushindi dhidi ya Uganda

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo Jumamosi, inatupa karata ya pili kwenye michuano ya Afcon 2025 pale itakapowakabili majirani zao Uganda katika mchezo mwingine wa kundi C.

Tanzania bado inasaka ushindi wa kwanza katika michuano hiyo na kuandika historia kwani hii ikiwa mara ya nne kufuzu kwa michuano ya Afcon, haijawahi kushinda.

Pengine ni nafasi sasa kwa Stars kuandikisha ushindi wake wa kwanza lakini haitakuwa rahisi mbele ya majirani zao Uganda.

Akizungumza mapema leo kuelekea mchezo huo, Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Miguel Gamondi, amesisitiza kuwa na imani kubwa na kikosi chake kuelekea mechi dhidi ya Uganda hapo kesho.

Gamondi amesema Taifa Stars imejiandaa vizuri na haina hofu dhidi ya The Cranes, akiamini uwezo, nidhamu na morali ya wachezaji wake vinaweza kuleta matokeo chanya katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye uwanja wa Al Medina.

Gamondi amesema heshima inatolewa kwa wapinzani wote, lakini Tanzania itaingia uwanjani kupambana kwa lengo la kushinda na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

“Uganda sio timu kubwa, wao na sisi ni kama sawa tu, angalia hata utofauti wa uwiano wa wachezaji wanaocheza ndani na nje, kisha utaona."

"Ni dabi na itakuwa mechi ngumu, lakini ubora na utendaji uwanjani utaamua mchezo. Kwa upande wetu tuna wachezaji wanaoweza kushinda huu mchezo tuna kina Msuva, Samatta; na hilo ni jambo ambalo watanzania wanapaswa kulifahamu,”  alisema Gamondi.

Tanzania na Uganda zitakutana huku zikiwa zimetoka kupoteza mechi zao za kwanza kundi C. Tanzania ilifungwa mabao 2-1 na Nigeria wakati Uganda wakichapwa mabao 3-1 na Tunisia.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’