Baada ya mapumziko ya sikukuu ya Christmas, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea mazoezini leo kuanza maandalizi ya michuano ya kombe la Mapinduzi.
Michuano ya kombe la Mapinduzi ilianza kutimua vumbi jana Disemba 28 kwa mchezo kati ya Singida Black Stars dhidi ya Mlandege ambao ulimalizika kwa Singida BS kuibuka na ushindi wa mabao 3-1
Yanga ni miongoni mwa timu zitakazoshiriki michuano hiyo ikiwa kundi C sambamba na TRA United na KVZ.
Yanga inatarajiwa kucheza mechi ya kwanza dhidi ya KVZ Januari 04 na kuhitimisha mechi ya pili ya makundi Januari 06 dhidi ya TRA United.
Ili kutnga nusu fainali, Yanga itahitaji kumaliza nafasi ya kwanza kutoka kundi C.
ADVERTISE HERE