Licha ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Comoros, timu ya Taifa ya Mali imepenya hatua ya mtoano Afcon 2025 ikikusanya alama 3.
Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra amecheza dakika zote 270 akilinda lango la Mali ambayo haijapoteza mchezo wala kushinda.
Aidha mshambuliaji Prince Dube nae aliitumikia Zimbabwe katika mechi zote tatu lakini haikuwa bahati upande wao kuvuka hatua ya mtoano.
Leo timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itakamilisha mechi ya tatu hatua ya makundi kwa mchezo dhidi ya Tunisia.
Tanzania inaweza kutinga hatua ya mtoano kama itaifunga Tunisia leo.
ADVERTISE HERE