Inaelezwa uongozi wa Yanga uko kwenye mazungumzo na Singida Black Stars kwa ajili ya uhamisho wa wachezaji Moussa Balla Conte na Mohamed Doumbia ambao wanatajwa kueleka Singida BS huku Yanga ikiwasajili Mohamed Damaro Camara na Marouf Tchakei.

Yanga imepania kuboresha kikosi chake katika dirisha hili dogo na wakati huu hakuna nafasi ya usajili wa kubahatisha.
Camara na Tchakei tayari wamecheza Tanzania kwa muda na hivyo hawatahitaji muda mrefu kuzoeana na wenzao kama ilivyotokea kwa Conte na Doumbia.
Aidha Yanga pia huenda ikamtoa kwa mkopo winga Ecua Celestin huku mshambuliaji Andy Boyeli akitarajiwa kurejea katika timu yake ya Shekhukhune United ya Afrika Kusini.
Jana Yanga ilithibitisha usajili wa mshambuliaji Emmenuel Mwanengo aliyetua kwa Wananchi akitokea klabu ya TRA United.
Nyota wengine ambao huenda wakajiunga na Yanga katika dirisha hili ni kiungo mshambuliaji Allan Okello na mshambuliaji Gerson Dala