Kikosi cha Yanga tayari kimerejea mazoezini kujiandaa na michuano ya kombe la Mapinduzi iliyoanza kutimua vumbi visiwani Zanzibar.
Yanga inatarajiwa kuelekea visiwani Zanzibar siku ya Jumamosi, January 03.
Mchezo wa kwanza utapigwa Jumapili, Januari 04 dhidi ya KVZ na kisha kumaliza mechi ya mwisho ya makundi siku ya Jumanne, Januari 06 dhidi ya TRA United.
Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves ataitumia michuano hiyo kama sehemu ya maandalizi ya kikosi chake wakati huu ambao ligi zimesimama kupisha michuano ya Afcon 2025 inayoendelea huko Morocco.
ADVERTISE HERE