Baada ya kumtambulisha kiungo Mohamed Damaro Camara, Yanga bado haijamaliza, kiungo mshambuliaji Marouf Tchakei nae anaelekea Jangwani.
Tchakei tayari yuko jijini Dar es salaam kukamilisha usajili wake na Yanga akikosa mchezo wa kombe la Mapinduzi, Singida BS ikichuana na Azam Fc.
Aidha nyota wa Yanga Mohamed Doumbia, Moussa Balla Conte nao huenda wakaelekea Singida BS kwa mkopo ikiwa ni sehemu ya makubaliano hayo.
Tchakei anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoshiriki michuano ya kombe la Mapinduzi.
ADVERTISE HERE