Mwanzo mzuri kwa nyota wapya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jan 2026
Mwanzo mzuri kwa nyota wapya Yanga

Nyota watatu wapya waliotua Yanga kwenye usajili wa dirisha hili dogo, unaweza kusema wameanza vyema majukumu yao kwenye kikosi cha Wananchi wote wakishiriki katika ushindi wa mabao 3-0 ambao Yanga waliupata dhidi ya KVZ katika mchezo wa kwanza kombe la Mapinduzi.

Mshambuliaji Emmanuel Mwanengo alipachika moja ya mabao ya Yanga katika mchezo huo ambao alicheza kwa dakika zote 90 huku Mohamed Damaro Camara 'Ngosha' akiingia dakika ya 61 kuchukua nafasi ya Duke Abuya na Mauruf Tchakei akichukua nafasi ya Ecua Celestin.

Mbali ya kufunga bao kwenye mchezo huo, Mwanengo alionekana kucheza kwa utulivu zaidi na kushirikiana vyema na wenzake.

Kwa ujumla, dakika zake tisini pasi yake moja tu aliyopiga ndio ilipotea, huku nyingine 21 zikifika kwa walengwa ambazo asilimia kubwa zilikuwa fupi.

Shuti moja alilopiga lilitoka nje ya boksi, huku akifanikiwa kuwania mpira wa juu mara moja ambapo kichwa alichopiga, hakikulenga goli.

Licha ya kuwa mshambuliaji wa mwisho, lakini kutokana na uwezo wake wa kucheza eneo la kiungo, Mwanengo alikuwa akishuka chini na kuifuata mipira kutoka kwa wenzake.

Upande wa Damaro aliyeingia kuchukua nafasi ya Duke aliyekuwa nahodha wa kikosi cha Yanga katika mchezo huo, aliendelea kuliweka eneo la kiungo katika utulivu mkubwa.

Kazi nzuri pia ilifanywa na Tchakei katika dakika chache alizocheza jambo lililomfurahisha mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves ambaye hata hivyo alisisitiza bado wachezaji hao watahitaji muda.

“Nina furaha kwa sababu kuna wachezaji wamecheza kwa mara ya kwanza na kufanya vizuri wakiwamo wawili kutoka timu ya vijana. Ninju (Abubakar Othuman) na George (Mzungu). Pia Damaro, Tchakei na Mwanengo. Wote wamefanya vizuri. Nimependa."

“Mwanengo ana wasifu wa kucheza kama winga, ni vizuri zaidi kwa sababu ni kawaida kwake kujifunza. Lakini pia anaweza kucheza kama mshambuliaji katika mfumo wa 4-4-2 au 4-3-3. Ana ujuzi mzuri."

“Kwa mechi hii nilimpa malengo yake, lakini tunakwenda hatua kwa hatua. Yote kwa yote nimeridhishwa na kiwango chake,” alisema Pedro baada ya dakika 90 za mchezo huo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
29m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
37m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’