Baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa katika michuano ya Afcon 2025, mshambuliaji Prince Dube amerejea nchini na leo anatarajiwa kuungana na kikosi cha Yanga Zanzibar.
Zimbabwe iliishia hatua ya makundi Afcon 2025 Dube akihusika katika mechi zote tatu huku akifunga bao moja.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amedokeza kuwa Dube atata Zanzibar na mshambuliaji mwingine mpya aliyesajiliwa na mabingwa hao wa nchi.
Mshambuliaji raia wa Angola Laurindo Dilson Aurelio 'Depu' kutoka klabu ya Radomiak Radom ya Poland anatajwa kujiunga na Yanga.
Habari njema nyingine kwa mashabiki wa Yanga ni kurejea kwa nyota wao waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho kinarejea nchini leo kutoka Morocco walikoondoshwa hatua ya 16 bora Afcon 2025.
Kama Yanga itatinga fainali ya kombe la Mapinduzi, ni waz nyota hao watakuwa sehemu ya kikosi kule dimba la Gombani, Pemba.