Kutoka Poland hadi Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jan 2026
Kutoka Poland hadi Jangwani

Mshambuliaji wa kimataifa wa Angola anayekipiga katika klabu ya Radomiak Radom ya Poland, Laurindo Aurelio 'Depú', anasubiri kutambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Yanga baada ya Mabingwa hao wa soka Tanzania Bara kwa misimu minne mfululizo kukamilisha usajili wake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mwandishi wa habari za michezo wa Poland, Szymon Janczyk, Yanga imefanikiwa kumsajili Depu kwa dau la euro 250,000 (zaidi ya 720M).

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Angola mwenye umri wa miaka 25 anatua kuungana na kocha wake wa zamani Pedro Goncalves ambaye anatajwa kupendekeza usajili wake.

Uhamisho huo unatarajiwa kuipatia Radomiak faida ya kifedha, huku pia wakiibana Yanga kutoa asilimia fulani ya mauzo ya baadaye.

Radomiak ilinunua mchezaji huyo kwa euro 100,000, pamoja na euro 100,000 nyingine kama bonasi kutoka klabu ya Gil Vicente ya Ureno.

Depu aliwasili katika soka la Poland majira ya kiangazi ya mwaka 2025, lakini alikumbana na changamoto za kiafya pamoja na ushindani mkubwa ndani ya kikosi, hali iliyopunguza muda wake wa kucheza.

Kwa jumla, alicheza takribani dakika 200, akishiriki mechi 10, akifunga bao moja na kutoa pasi moja ya goli. Katika timu ya Taifa ya Angola, Depu amefunga mabao 15 katika mechi 18 chini ya Goncalves.

Goncalves ndiye aliyempa Depu nafasi ya kuanza kucheza katika kikosi cha kwanza cha Angola. Uhusiano wao wa awali katika timu ya Taifa ya Angola una mchango mkubwa katika kukamilika kwa usajili huo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’