Klabu ya Yanga imetangaza rasmi mwito wa kuwasilisha barua ya kuonesha nia (EOI) kwa wawekezaji na wabia wa kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa eneo la Jangwani/Twiga Street jijini Dar es Salaam.
Uwanja huo unapangwa kuwa na uwezo wa watazamaji 25,000–35,000, ukiwa na hybrid pitch, maeneo ya VIP, mifumo ya kisasa ya usalama, taa, umwagiliaji na miundombinu ya kibiashara.
Yanga iko tayari kuingia ubia kupitia mifumo mbalimbali ikiwemo Naming Rights, Sponsorship-led funding, PPP na DBFO, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha mapato na maendeleo ya klabu kwa muda mrefu.
arehe ya mwisho ya kuwasilisha EOI: Januari 23, 2026, saa 10:00 jioni. Hatua hii inaonesha dhamira ya Yanga ya kujenga uwanja wa kisasa wa viwango vya kimataifa na kuendelea kuimarisha hadhi ya klabu kitaifa na kimataifa.