Jumatatu, Januari 19 2026 Yanga itaendelea na kampeni ya kusaka ubingwa wa tano mfululizo ligi kuu ya NBC pale itakapoikaribisha Mashujaa Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex.
Wananchi wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na alama 16 baada ya ya mechi 6, ushindi katika mchezo huo unaweza kuwapeleka kileleni mwa msimamo wa ligi kwa mara ya kwanza msimu huu.
Na Yanga inapokaa kileleni mwa msimamo sio jambo jepesi kuwaondoa katika nafasi hiyo kwani hata pale wanapoondoka, ni suala la muda tu hurejea tena juu.
Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na maboresho ya kikosi yaliyofanyika katika dirisha hili dogo.
Licha ya nyota wapya hasa Depu na Allan Okello kupata siku chache za kufanya mazoezi na timu, wanaonekana wako 'fit' na tayari kutumika kwenye kikosi cha kwanza.
Baada ya mchezo huo Yanga itapeleka nguvu zake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa wakikabiliwa na mchezo dhidi ya Al Ahly ugenini Januari 23.