Al Ahly yaipeleka Yanga Alexandria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jan 2026
Al Ahly yaipeleka Yanga Alexandria

Ijumaa ya Januari 23 2026 Yanga itakuwa uwanjani huko Misri kumenyana na mabingwa wa kihistoria ligi ya mabingwa barani Afrika, Al Ahly katika mchezo wa raundi ya tatu kundi B.

Wenyeji Al Ahly wamechagua kupeleka mchezo huo Uwanja wa Borg El Arab uliopo Alexandria ikiwa ni mwendo wa wastani wa saa nne kutoka Cairo kwa usafiri wa treni au basi.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Yanga kuikabili Al Ahly katika uwanja huo kwani mwaka 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi CAFCL, Yanga ilipoteza kwa mabao 2-1 mchezo wa marudiano baada ya awali kutoka sare ya bao 1-1 jijini Dar es salaam.

Uwanja huo umekuwa ukitumiwa na Al Ahly na wapinzani wao, Zamalek kwenye baadhi ya mechi badala ya Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, ambao hutambulika kama uwanja wao wa Taifa.

Ni desturi za timu za Misri kutumia uwanja huo wa pili kwa ukubwa nchini humo kwa ajili ya kuwapelekea mechi mashabiki wa soka wa Kaskazini mwa Misri, na ni wa kisasa wenye urefu wa mita 105 na upana wa mita 70 eneo la kuchezea.

Uwanja huo upo kilomita 1.5 kutoka kituo cha treni na umbali wa kilomita 15 kutoka Alexandria mjini, ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 86,000 walioketi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’