Jana mashabiki wa Yanga walimshuhudia mshambuliaji wao mpya Laurindo Dilson Maria Aurelio 'Depu' kwa mara ya kwanza katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc.
Licha ya kucheza kwa takribani dakika 20 tu, Wananchi walitoka uwanjani na nyuso za furaha baada ya kile walichokishuhudia kutoka kwa Depu katika mchezo huo.
Ni mapema kutabiri nini Depu atafanya akiwa na uzi wa Yanga lakini waswahili wana msemo wao 'Siku njema huonekana asubuhi'.
Asubuhi hiyo ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa, ikiwa siku yake ya kwanza akiitumikia Yanga, Depu akafunga bao na kutoa pasi nyingine ya bao.
Depu ameonyesha ni aina ya mshambuliaji ambaye hakuna beki anatamani kukutana nae.
Ni msumbufu, ana nguvu, kasi na maarifa, dakika chache alizocheza dhidi ya Mashujaa Fc, aliwaweka kwenye wakati mgumu walinzi wa timu hiyo.
Bila shaka Depu atakuwa msaada mkubwa kwa Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na pengine atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Al Ahly Ijumaa ya wiki hii kule Misri