Ecua, Doumbia ndio basi tena

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jan 2026
Ecua, Doumbia ndio basi tena

Nyota wawili wa Yanga kiungo Mohamed Doumbia na winga Ecua Celestin hawajajumuishwa katika kikosi kilichoondoka Alfajiri ya leo kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa siku ya Ijumaa.

Yanga iko kwenye mchakato wa kuwatoa wachezaji hao kwa mkopo na hivyo tayari wameondolewa kwenye mipango ya kocha Pedro Goncalves.

Mpango wa awali wa kuwapeleka Singida BS ni kama umekuwa mgumu kwa upande wa wachezaji. Taarifa za ndani zimedokeza kuwa klabu ya Sekhukhune United ya Afrika Kusini imeonyesha nia ya kuwasajili nyota hao.

Kama mpango huo utakamilika basi wataungana na mshambuliaji Andy Boyeli ambaye amerejea timu hiyo baada ya mkataba wake wa mkopo kusitishwa.

Boyeli, Ecua na Doumbia wamewapisha Allan Okello, Depu na Yao Kouassi kwenye kikosi.Β 

Baada ya kung'ara kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi, kiungo Moussa Balla Conte amenusurika na mpango wa kutolewa kwa mkopo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’