Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly utakaopigwa kesho Ijumaa, Januari 23 katika uwanja wa Borg El Arab yanakwenda vizuri.
Licha ya baridi kali katika mji wa Alexandria, Kamwe amesema timu iliwasili salama jana na wakapata nafasi ya kufanya mazoezi yao kwa kwanza.
Kamwe amesema leo kikosi kitakamilisha maandalizi katika dimba la Borg El Arab ambapo mchezo huo utapigwa hapo kesho.
"Tunamshukuru Mwenye ez Mungu tumewasili salama hapa Alexandria wachezaji wote wako katika hali nzuri."
"Hali ya hewa hapa ni baridi kali inayofikia nyuzi joto 17, naamini wachezaji wetu watazoea haraka kwani sio mara ya kwanza kukutana na mazingira ya aina hii."
"Tulikwenda Algeria hali ya hewa ilikuwa chini ya nyuzi joto 13 lakini vijana wetu walipambana na tukapata matokeo mazuri."
"Leo kutakuwa na mkutano na wanahabari, kocha Pedro Goncalves ataongozana na Allan Okello kuzungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya mchezo huo."
"Tutakamilisha maandalizi yetu jioni muda wa mchezo, nisema tu timu yetu iko tayari kwa mechi hii muhimu dhidi ya Al Ahly," alisema Kamwe