Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema wamewasili salama Nakuru, Kenya tayari kwa mashindano ya SportPesa Super Cup yanayoanza keshokutwa Juni 03.
Yanga itafungua mashindano hayo kwa kucheza na Kakamega HomeBoyz keshokutwa, mchezo ukitarajiwa kupigwa saa saba mchana.
Mshindi wa mchezo huo atatinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa atajinyakulia kitita cha Mil 68 pamoja na tiketi ya kwenda kucheza na Everton katika dimba la Goodison Park nchini Uingereza.
Saleh amewataka mashabiki wa Yanga kuungana pamoja, kuiombea dua timu yao iweze kufanya vizuri kwenye michuano.
Naye Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu amesema wachezaji wote 20 waliosafiri jana wako kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo wa keshokutwa.

ADVERTISE HERE