Klabu ya Yanga imetoa pole kwa familia wa mlinda lango wa zamani wa timu hiyo Peter Manyika aliyefariki dunia leo.
Manyika amefariki dunia mapema leo Januari 26, 2026 akiwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya St. Monica jijini Dar es Salaam.
"Uongozi wa Klabu yetu, Wanachama na Mashabiki kwa ujumla tumepokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa na tunaungana na familia katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo."
"BWANA alitoa na BWANA ametwaa jina la BWANA lihimidiwe," ilisema taarifa ya Yanga

ADVERTISE HERE