Kiungo mshambuliaji wa Yanga Celestin Ecua yuko mbioni kujiunga na klabu ya JS Kabylie ya Algeria, imefahamika.
Ecua anatarajiwa kutua Kabylie kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Yanga tayari imemuondoa Ecua kwenye mipango yake, awali alikuwa akihusishwa kutua klabu ya Sekhukhune United Afrika Kusini sambamba na Mohamed Doumbia ambaye pia hayuko kwenye mipango ya kikosi cha Wananchi.
Yanga imeongeza nyota watatu wa kigeni kwenye dirisha dogo ambao ni Depu, Allan Okello na Yao Kouassi huku ikiachana na And Boyeli, Doumbia na Ecua.
Ecua huenda akaikabili Yanga kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa timu hizo zitakapokutana mechi ya kuhitimisha hatua ya makundi, kundi D
ADVERTISE HERE