Yanga yajipanga kumpa Dube mkataba mpya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jan 2026
Yanga yajipanga kumpa Dube mkataba mpya

Uongozi wa Young Africans SC (Yanga) umeanza kuchukua tahadhari mapema ili kumhakikishia mshambuliaji wao tegemeo, Prince Dube, anaendelea kusalia ndani ya kikosi hicho hata baada ya msimu huu kumalizika.

Dube, aliyesajiliwa na Yanga mwanzoni mwa msimu wa 2024/2025 akitokea Azam FC, alisaini mkataba wa miaka miwili unaotarajiwa kufikia tamati yake mwezi Juni 2026. Hata hivyo, muda uliosalia katika mkataba huo ni chini ya miezi sita, hali iliyowalazimu mabosi wa Jangwani kuanza hatua za mapema.

Umaarufu wa mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe umeongezeka zaidi kufuatia kiwango kizuri alichoonyesha katika AFCON 2025, ambapo alifanikiwa kufunga bao moja licha ya timu yake kutofuzu hatua ya 16bora. Dube amezivutia klabu kadhaa kutoka nje ya nchi, hususan Saudi Arabia na Morocco, ambazo zimeanza kuonyesha nia ya kumnasa straika huyo.

Chanzo cha ndani kimenukuliwa kikisema kuwa mkakati wa Yanga ni kuwahi kukaa mezani na wachezaji muhimu kabla ya msimu kumalizika, ili kuepuka hatari ya kuwapoteza bure. Mbinu hii imewahi kuzaa matunda hapo awali kwa nyota kama Pacome Zouzoua, Kouassi Attohoula Yao na hata Djigui Diarra, ambao mikataba yao iliongezwa kabla ya muda wake kuisha.

Kwa upande wa takwimu, Dube ameendelea kuwa silaha muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Yanga. Ndani ya misimu miwili, amefunga jumla ya mabao 16 katika Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo msimu wake wa kwanza aliibuka na mabao 13, huku msimu wa sasa akiwa ameweka kambani mabao matatu hadi sasa.

Mbali na Dube, Yanga pia inakabiliwa na changamoto ya mikataba ya wachezaji wengine wanaokaribia ukingoni, akiwemo Chadrack Boka, Kibwana Shomari na Farid Musa, jambo linaloifanya klabu hiyo kuingia katika kipindi muhimu cha kupanga mustakabali wa kikosi chake.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’