Mshambuliaji mpya wa Yanga Laurindo Dilson Maria Aurelio 'Depu' ameanza majukumu yake ndani ya kikosi cha Wananchi na gia kubwa jana akiwaongoza Wananchi kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji.
Katika mchezo huo ambao Depu aliibuka na tuzo ya nyota wa mchezo, aliweka kambani mabao mawili na kuendeleza rekodi tamu katika mechi yake ya pili.
Depu sasa amepachika mabao matatu huku akiwa na asisti moja, bao alilotengeneza katika mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa Fc.
Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka kwa ushindi wa mabao 6-0, Depu pia alifunga bao moja.
Wakati Yanga ilipotambulisha usajili wake, kuliibuka mjadala juu ya takwimu zake za mabao huko alikotoka.
Bila shaka mjadala huo sasa umekufa 'kifo cha mende' kwani kuna kila dalili anaweza kuweka rekodi msimu huu kama ataendelea na kasi yake ya kufunga kila mechi.
