Maswali yamekuwa mengi kutoka kwa Wananchi juu hatma ya kiungo mshambuliaji Celestin Ecua ambaye amejiunga na JS Kabylie kwa mkopo akitokea klabu ya Yanga.
Mwezi ujao Yanga itakuwa mwenyeji wa JS Kabylie katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).
Imethibitishwa Yanga na JS Kabylie wana makubaliano ya kimkataba juu ya Ecua kutocheza mchezo huo dhidi ya waajiri wake.
Ikumbukwe licha ya kutua Kabylie Ecua bado ni mwajiriwa na Yanga hadi pale JS Kabylie watakapomsajili moja kwa moja kama wataridhishwa na kiwango chake.
Hivyo katika mchezo dhidi ya Yanga, Ecua atakaa jukwaa kushuhudia mtanange huo. Lakini Kabylie wanaweza kumtumia katika mechi zao mbili dhidi ya AS FAR na Al Ahly na wamemjumuisha katika kikosi kilichosafiri Morocco kuifuata AS FAR.