Tuko tayari kuikabili Al Ahly - Goncalves

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jan 2026
Tuko tayari kuikabili Al Ahly - Goncalves

Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly yamekamilika kikosi chake kikiwa tayari kukabiliana na mabingwa hao wa kihistoria Afrika.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Goncalves amesema wanakwenda kwenye mchezo huo kwa tahadhari kubwa huku dhamira yao ikiwa kuibuka na ushindi.

Goncalves amesema Al Ahly wana wachezaji wengi wenye ubora na uzoefu mkubwa, wanaweza kukuadhibu kwa kila kosa utakalofanya.

Amesema wamejiandaa kwenda kukabiliana nao huku wakiweka mkazo kwenye umakini wanapokuwa na mpira na hata bila ya mpira.

"Tayari tumeshafanya maandalizi yetu uwanjani na sasa tunaendelea na maandalizi mengine. Kama mchezo ungekuwa leo basi naweza kusema kikosi kipo tayari, tupo tayari kuwa na mchezo mzuri kesho huku tukiwaheshimu wapinzani wetu kwakuwa na wao wana timu nzuri"

"Kabla ya yote tulipopangwa kwenye kundi hili kila timu ilifahamu ipo kwenye kundi gumu, sisi kama Young Africans kazi yetu ni kupambana na kila timu ili kujiweka kwenye sehemu nzuri tunapaswa kuwa bora, makini na tayari kucheza mpira mzuri ili kuwa sehemu nzuri"

"Kuhusu mechi ya kwanza ni kweli tulicheza vizuri lakini tulifanya makosa machache ambayo kwa ubora wa wapinzani wetu walituadhibu. Hapo kesho tunapaswa kuonesha ukuaji na ubora wetu pia ili kushinda"

"Tunaamini tunashindana na timu kubwa, tunajua kesho kutakuwa na nyakati tofauti, kuna muda tutakuwa na Mpira na kuna muda na wao watakuwa na Mpira, kuna muda tutafanya mashambulizi na wao pia watafanya hivyo, tunatakiwa kuwa makini katika kila nyakati ili tutimize lengo letu la kushinda," alisema Goncalves

Akiwazungumzia Al Ahly, Goncalves amesema kukosekana kwa kiungo Emam Ashour ni pigo kwao lakini upande wa kikosi chake hilo sio jambo la kulifurahia kwa sababu Al Ahly wana wachezaji wengi wanaoweza kutumika nafasi ya Ashour.

"Wao kumkosa Emam Ashour ni pigo kwao lakini kwetu hatuwezi kusema ni faida moja kwa moj. Zizo huwa anacheza sana pale kwenye timu ya Taifa na hata alipoumia Emam yeye ndiye alicheza. Ni lazima tujiangalie sisi wenyewe kwanza, wale wana watu wenye uwezo mkubwa," aliongeza Goncalves

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’