Kikosi cha Yanga leo Jumanne itaondoka nchini kuelekea Morocco kwa ajili ya mchezo wa raundi ya tano CAFCL dhidi ya AS FAR ya nchini humo.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi Februari 07, saa 4 usiku kwa saa za Tanzania.
Yanga inasafiri Morocco mapema kwa kutambua umuhimu wa mchezo huo ambao unabeba matumaini ya kufuzu robo fainali.
Ushindi au sare ndio matokeo ambayo Wananchi wanahitaji ugenini katika mpango wao wa kuisaka tiketi ya robo fainali.
ADVERTISE HERE