GSM yashinda tenda ya ujenzi wa uwanja Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Feb 2026
GSM yashinda tenda ya ujenzi wa uwanja Jangwani

Kampuni ya GSM imeshinda tenda ya ujenzi wa uwanja wa Yanga Makao Makuu ya klabu Jangwani jijini Dar es salaam.

Kamati ya Utendaji ya Yanga ilikutana siku ya Jumamosi kupitia maombi ya Wazabuni mbalimbali na hatimaye GSM kuibuka mshindi baada ya kukishi vigezo vilivyowekwa.

GSM ametangazwa leo katika Mkutano na Wanahabari uliofanyika Makao Makuu ya Yanga, Jangwani mapema leo.

Kabla ya kumtangaza GSM, uongozi wa Yanga ulieleza masikitiko yake na kukemea vurugu alizofanyiwa Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu na mashabiki wa timu hiyo baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Esperance uliopigwa jana na kumalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2.

Kwa niaba ya uongozi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alitangaza maamuzi yaKamati ya utendaji kuichagua kampuni ya 

“Kabla sijaenda kwenye Agenda iliyotuleta leo hii, Uongozi wa Young Africans umenituma kuwaeleza haya yafuatayo, Jana tumeona Video nyingi zikiwaonesha Mashabiki kumvamia mwenyekiti wa Klabu ya Simba Sports Club Murtaza Mangungu, Young Africans tunakemea na kupinga vikali vitendo vya kihuni vilivyofanyika hapo jana, hata hivyo tunampa Pole Mwenyekiti pamoja viongozi wengine waliyopatwa na Kadhia ile”

“Siku ya Jumamosi uongozi wetu ulikaa kikao cha kamati ya Utendaji inayoongozwa na Rais Eng. Hersi Ally Said na kujadili agenda moja ya Msingi ya Mchakato wa ujenzi wa uwanja wa Young Africans Sports Club, Kikao kile kilikwenda kutoa majibu ya kampuni au Taasisi iliyoshinda Tenda ya kushirikiana na Yanga kwenye ujenzi wa uwanja wa Yanga.

“Kabla hatujamtaja mshindi wa Tenda hii naomba niwapitishe kwenye mchakato mzima wa Ujenzi wa Uwanja huu, Mchakato huu umepita kwenye hatua mbali mbali, hatua ya kwanza ilikuwa kufanya Tathmini ya eneo la ujenzi wa uwanja, baadae tukagundua kuwa kuna Eneo la ziada linahitajika kwenye kukamilisha ujenzi huo, baadae tukashirikiana na Serikali kuomba eneo la ziada. Hapa nichukue Fursa hii kuishukuru Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia Eneo la ziada"

“Nichukue Fursa hii kuwatangazia Watanzania, Kampuni ya GSM TANZANIA LIMITED ndiyo iliyoshinda tenda ya Ujenzi wa Uwanja wa Young Africans Sports Club"

"Viongozi wetu wakiongozwa na Rais wa Klabu walikuwa na ndoto ya kujenga uwanja, wakaamua kuwa uwanja ujengwe makao makuu ya klabu yetu. Wakashauriwa na wataalamu. Lakini wakagundua lazima wapate nyongeza ya ardhi ili uwanja wetu ukidhi matakwa CAF. Serikali ikatupatia eneo na Hati tunayo na baada ya mchakato huo tukatafuta mkandarasi ambaye atatujengea uwanja. Hatimaye GSM Tanzania LTD wameshinda tenda hii,” alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’