Goncalves aweka mkakati wa kuikabili AS FAR

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Feb 2026
Goncalves aweka mkakati wa kuikabili AS FAR

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema amekiandaa kikosi chake kimbinu kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS FAR utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Olympic huko Morocco.

Akizungumza mapema leo katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Goncalves alisema anatambua ubora wa AS FAR, hivyo amekiandaa kikosi chake kukabiliana nao kwa kulingana na vile watakavyokuja.

"Tunawajua wapinzani wetu wana timu nzuri ambayo wanaweza kucheza katika mazingira tofauti ya kimbinu. Tumejiandaa kuwakabili kwa namna yoyote ambayo watakuja nayo."

"Hakuna timu bora ambayo haina madhaifu, tutatumia madhaifu yao kupata matokeo. Tuna timu bora ya kupata matokeo katika mazingira magumu".

"Tumekuwa na wakati mzuri pamoja na maandalizi mazuri na tumekuwa na mwendelezo mzuri wa kutengeneza nafasi kwenye michezo yetu na tunaamini kesho tutaendelea kufanya hivyo."

"Tunawaheshimu wapinzani wetu, wana kikosi kizuri kuanzia kwenye safu ya ulinzi mpaka safu yao ya ushambuliaji na ni moja ya Klabu kubwa hapa Morocco. Lakini tunaamini kesho tuna nafasi ya kufanya vizuri na tunatakiwa kutumia nafasi zetu kwa usahihi na umakini mkubwa," alisema Goncalves

Yanga inatarajiwa kukamilisha maandalizi ya mwisho leo kwenye dimba la Olympic tayari kwa mtanange huo ambao Wananchi wanaweza kusafisha njia ya kutinga robo fainali kama wataibuka na ushindi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’