Novemba 05 2025 mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize alifanyiwa upasuaji wa goti ambao ulimlazimu kuwa kwenye matibabu kwa takribani wiki 12.
Hatimaye jana alirejea kikosini akipata nafasi ya kucheza dhidi ya AS FAR katika mchezo wa raundi ya tano hatua ya makundi CAFCL Yanga ikikubali kichapo cha bao 1-0 huko Morocco.
Mzize aliingia akichukua nafasi ya Pacome Zouzoua ambaye unaweza kusema AS FAR walimuwekea mkakati madhuburi wa kumzuia.
Kurejea kwa Mzize ni habari njema kwa kocha Pedro Goncalves kwani sasa atakuwa na machaguo zaidi kwenye safu yake ya ushambuliaji.



ADVERTISE HERE