Mabingwa wa kihistoria wa soka Tanzania, Yanga kesho Jumapili Juni 03 2018 wanashuka kwenye uwanja wa Afraha huko Nakuru nchini Kenya kuikabili Kakamega HomeBoyz kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup.

Leo inatarajiwa kufanya mazoezi yake ya mwisho kabla ya mchezo huo ambao mshindi atatinga hatua ya nusu fainali.
Nahodha wa Yanga Thabani Kamusoko amesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili kuwezo kutimiza lengo la kuondoka na taji la mashindano hayo.
Yanga iliondoka na kikosi cha wachezaji 20 lakini imeelezwa wachezaji wengine wanaweza kusafiri kwenda kuongeza nguvu baada ya mchezo wa kesho iwapo Yanga itafuzu hatua ya nusu fainali.
Mchezo huo utapigwa saa saa mchana.

ADVERTISE HERE