Kikosi cha Yanga kimerejea usiku wa kuamkia leo baada ya safari ndefu ya kutoka Morocco wakipitia Lagos Nigeria, Accra Ghana na moja kwa moja Dar es salaam.
Yanga ina takribani siku nne za kukamilisha maandalizi yake kabla ya kuikabili JS Kabylie katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi siku ya Jumapili.
Ni mchezo wa maamuzi ambao ushindi unaweza kuipeleka Yanga hatua ya robo fainali.





ADVERTISE HERE