Iliwezekana dhidi ya CR Belouizdad, itawezekana dhidi ya JS Kabylie

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Feb 2026
Iliwezekana dhidi ya CR Belouizdad, itawezekana dhidi ya JS Kabylie

Katika misimu minne mfululizo, Yanga imejikuta ikikabiliana na timu kutoka Algeria katika hatua za maamuzi za michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika. Kila msimu umebeba simulizi yake, maumivu yake na matumaini yake.

Msimu wa 2022/23, Wananchi walikutana na USM Alger katika fainali ya Kombe la Shirikisho. Baada ya sare ya jumla ya mabao 2-2 katika mechi mbili, Yanga ilikosa ubingwa kwa kanuni ya mabao ya ugenini. Walifungwa 2-1 nyumbani kabla ya kushinda 1-0 ugenini, ushindi ambao haukutosha kubeba kombe, lakini ulionyesha uwezo na uthabiti wao katika anga la Afrika.

Msimu uliofuata wa 2023/24, wakakutana tena na ukuta wa Algeria, safari hii dhidi ya CR Belouizdad katika hatua ya maamuzi ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa. Yanga ilihitaji ushindi wa mabao 4-0 ili kufuzu kazi iliyoonekana kuwa nzito.

Lakini katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Wananchi wakaandika historia. Mabao ya Mudathir Yahya, Kennedy Musonda, Stephane Aziz Ki na Joseph Guede yaliihakikishia Yanga ushindi wa 4-0 na tiketi ya robo fainali. Ilikuwa ni usiku wa kumbukumbu, ushahidi kwamba hakuna lisilowezekana kwa dhamira na umoja.

Msimu wa 2024/25, Yanga ilihitaji tena ushindi dhidi ya MC Alger ili kuvuka hatua ya robo fainali. Hata hivyo, safari hii mambo hayakuenda kama ilivyotarajiwa. Mchezo uliochezwa Benjamin Mkapa ulimalizika kwa sare ya 0-0, matokeo yaliyokatisha ndoto za kusonga mbele.

Sasa, msimu huu, historia inajirudia. Kwa mara nyingine tena, Wananchi wanakutana na timu kutoka Algeria, JS Kabylie. Ili kutinga robo fainali, Yanga inahitaji ushindi wa angalau mabao 2-0, huku wakisubiri pia matokeo ya mchezo kati ya Al Ahly na AS FAR. Ushindi wa Al Ahly utawapa Wananchi nafasi kubwa ya kufuzu.

Hata hivyo, jukumu la kwanza na la msingi liko mikononi mwao wenyewe: kushinda mechi yao. Mengine yatafuata baada ya dakika 90 kukamilika.

Njia ni ileile waliyoipita dhidi ya CR Belouizdad misimu miwili iliyopita, wanahitaji imani, umakini na uthubutu. Tofauti ni uwanja pekee. Safari hii, kazi hiyo inapaswa kukamilishwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, Jumapili majira ya saa 1 usiku.

Itawezekana!, huu ni wakati mwingine kwa Yanga kuvuka kigingi kingine cha timu kutoka Algeria na kuandika rekodi nyingine barani Afrika kwa kufuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’