Yanga imepania kufuzu kwa kishindo Zanzibar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Feb 2026
Yanga imepania kufuzu kwa kishindo Zanzibar

Klabu ya Yanga SC imejipanga kumaliza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kwa kishindo, ikihitaji ushindi wa mabao angalau 2-0 dhidi ya JS Kabylie katika mchezo wa mwisho wa Kundi B utakaochezwa Jumapili, Februari 15, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Katika msimamo wa sasa wa Kundi B, Al Ahly wanaongoza wakiwa na alama 9, wakifuatiwa na AS FAR wenye alama 8. Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 5, huku JS Kabylie wakishika mkia kwa alama 3.

Ili kutinga robo fainali, Yanga inalazimika kushinda mechi yake kwa tofauti ya mabao mawili au zaidi, huku ikiomba Al Ahly waibuke na ushindi dhidi ya AS FAR bila kuruhusu bao katika mchezo wao utakaopigwa Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, Misri.

Kwa mujibu wa takwimu za kundi hilo, Yanga hadi sasa imefunga mabao mawili na kuruhusu manne, wakati AS FAR wamefunga matatu na kuruhusu mawili. Endapo Yanga itafunga mabao mawili au zaidi na AS FAR wakapoteza bila kufunga, Yanga itakuwa imefikisha idadi kubwa zaidi ya mabao ya kufunga, jambo litakaloipa tiketi ya robo fainali kwa kuzingatia kanuni za mashindano.

Katika rekodi za michezo ya ana kwa ana (head-to-head), Yanga na AS FAR wanalingana baada ya kila timu kushinda 1-0 nyumbani kwake. Hivyo, ushindi mnono kwa Yanga pamoja na matokeo mazuri kutoka Cairo unaweza kuwa tiketi ya kihistoria kwa wawakilishi hao wa Tanzania.

Mchezo wa Zanzibar unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa, huku Yanga ikitegemea nguvu ya mashabiki wake katika dimba la New Amaan Complex. Kauli mbiu ya timu hiyo kuelekea pambano hilo ni “Tunafuzu kwa Kishindo,” ikionyesha dhamira ya kuvuka hatua hiyo kwa namna ya kipekee.

Akizungumza kuelekea mchezo huo wa maamuzi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, alisema timu hiyo ina sababu ya kuamini katika kauli mbiu hiyo kutokana na hadhi ya timu zilizopo kwenye kundi hilo.

“Tupo katika kundi ambalo timu tatu zimewahi kuwa mabingwa wa Afrika, isipokuwa Yanga tu. Sasa tunasema tunakwenda kufuzu kwa kishindo kwa sababu tukifanikiwa tutavuka mbele ya timu bingwa, yaani tutakwenda robo fainali na bingwa mmoja na kuwaacha wengine wawili. Huko ndio kufuzu kwa kishindo!,” alisema Kamwe.

Upande wa pili wa kundi, Al Ahly wanatarajiwa kuwa na sapoti kubwa ya mashabiki wao baada ya kuruhusiwa kujaza Uwanja wa Kimataifa wa Cairo. Miamba hiyo ya Misri inahitaji ushindi au sare ili kumaliza kinara wa Kundi B, lakini ushindi wao ndio matokeo yatakayofungua mlango kwa Yanga iwapo nayo itatimiza wajibu wake Zanzibar.

Hatima ya Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika sasa iko mikononi mwao, huku macho ya mashabiki wa soka nchini yakielekezwa Zanzibar na Cairo kwa wakati mmoja. Jumapili hii inaweza kuwa siku ya historia kwa Wananchi iwapo watatimiza hesabu zao na kufuzu kwa kishindo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’