Mtibwa Sugar Bingwa ASFC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jun 2018
Mtibwa Sugar Bingwa ASFC
Wakatamiwa wa Mtibwa Sugar wametwaa kombe la FA (ASFC) baada ya kuilaza Singida United mabao 3-2 kwenye mchezo wa fanali uliopigwa katika dimba la Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Mtibwa Sugar ilipata mabao yake kupitia kwa Salum Kihimbwa 22', Issa Rashid 37' na Ismail Mheja 90' wakati yale ya Singida United yalipachikwa na Salum Chukwu 43' na Tafadzwa Kutinyu 70'.



Mchezo huo ulikuwa na upinzani mkali kutoka kila upande, Singida United ikitawala kwa muda mwingi lakini Mtibwa Sugar ikiwa na madhara zaidi langoni kwa Singida United.

Mtibwa Sugar ilimaliza na wachezaji 10 uwanjani baada ya mfungaji wake wa bao la pili Issa Rashid 'Baba Ubaya' kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 78 kwa kuonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumtolea lugha chafu mwamuzi.



Ushindi huo umeipa Mtibwa Sugar nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao huku ikijinyakulia kitita cha Mil 50.

Mchezo huo pia umehitimisha vibaya msimu wa kocha wa Singida United Hans van Pluijm anayekwenda kujiunga na Azam FC.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’