Mashabiki wa Yanga bado hawajamshuhudia nyota wao mpya Buba Jammeh aliyetua siku ya mwisho ya usajilli wa dirisha dogo.
Huenda leo Wananchi wakapata nafasi ya kumshuhudia kwa mara ya kwanza katika mchezo wa hatua ya 64 bora kombe la CRDB dhidi ya Cosmopolitan.
Buba alijumuishwa kwenye kikosi cha mechi iliyopita ya ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie lakini hakutumika katika mchezo huo.
Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves alihitaji Buba kupata muda wa kufanya mazoezi na wenzake kabla yak kuanza kutumika rasmi.
Yanga inahitaji kuanza vyema michuano ya CRDB wakiwa ni mabingwa watetezi wakitwaa taji hilo kwa misimu minne mfululizo.
ADVERTISE HERE