Kamwe afunguka Yanga kucheza chini ya kiwango dhidi ya Cosmopolitan

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Feb 2026
Kamwe afunguka Yanga kucheza chini ya kiwango dhidi ya Cosmopolitan

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cosmopolitan katika mchezo wa hatua ya 32 bora kombe la CRDB, ni matokeo muhimu kwao kwani wamekata tiketi ya kufuzu hatua ya 32 bora.

Kamwe amesema lengo lao kwenye mchezo huo ilikuwa ushindi na kusonga mbele bila ya kujali idadi ya mabao waliyofunga.

Kamwe ametoa kauli hiyo kuwajibu wale waliobeza ushindi huo wakiamini Yanga ilipaswa kufunga mabao mengi dhidi ya timu hiyo inayoshiriki ligi ya Championship.

Msemaji huyo wa mabingwa wa nchi amesema Yanga imetoka kucheza mechi ngumu za ligi ya mabingwa na pia wakikabiliwa na mfululizo wa mechi hivyo ilikuwa muhimu kwa benchi la ufundi na wachezaji kuchukua tahadhari.

"Nimeona maoni ya watu wengi walitaka tufunge mabao mengi, huo sio mpira wa miguu. Tumetoka kwenye mechi ngumu Jumapili, tumerudi Jumatatu kwa maana yake tumefanya mazoezi siku moja tu na kwa asilimia kubwa wamecheza wale wale waliotumika Jumapili."

"Hizi ni mechi za kurefresh, cha muhimu unapata matokeo unakwenda kwenye hatua inayofuata. ‎Tuna mechi nyingine, Jumapili dhidi ya Namungo kule Ruangwa lakini pia tutakuwa na mechi tarehe 25 dhidi ya JKT hapa KMC Complex."

"Kwahiyo ni lazima wachezaji wetu wacheze kwa umakini mkubwa ili pia kujiepusha na majeraha na ndio maana wamecheza kwa tempo ya kawaida," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’