Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga walirejea mazoezini jana kujiandaa na mechi zinazofuta kwenye ligi kuu ya NBC.
Leo Wananchi watakamilisha maandalizi yao jijini Dar es salaam ambapo kesho Jumamosi watasafiri kuelekea mkoani Lindi tayari kwa mchezo dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa Jumapili, Februari 22 katika uwanja wa Majaliwa, Ruangwa.
Baada ya mchezo huo Yanga itarejea Dar kuikabili JKT Tanzania Februari 25 mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex na kisha kuelekea visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa March 1 katika uwanja wa New Amaan Complex.
Ni ratiba ya mechi mfululizo kwani baada ya mchezo dhidi ya Simba, Wananchi watasafiri hadi mkoani Singida kuikabili Singida Black Stars March 05
ADVERTISE HERE