Jumapili Februari 22 Yanga itakuwa ugenini uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc.
Wenyeji wa mchezo huo Namungo wametangaza viingilio vya mtanange huo utakaopigwa kuanzia saa 1 usiku. Mzunguuko ni Tsh 5,000/- na jukwaa kuu ni Tsh 20,000/-
Yanga inatarajiwa kuondoka jijni Dar es salaam kesho Jumamosi kwa usafiri wa ndege ambapo pia msafara wa mashabiki wa jijini Dar es salaam nao wataondoka na mabasi.

ADVERTISE HERE